Friday, May 22, 2015

JINI KABULA & SHERMAN PROJECT YA MAHABA MAZITO Muigizaji wa Bongo Muvi, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula.

Straika wa Yanga, Kpah Sherman.

Nicodemus Jonas na
Musa Mateja

LICHA ya kuwa na muda mfupi tangu atue nchini kucheza soka akitokea nchini Cyprus, straika wa Yanga, Kpah Sherman amekuwa akiandamwa na matukio ya ajabu.

Awali alipoanza kazi alionyesha uwezo wa juu katika mechi dhidi ya Simba ya Mtani Jembe lakini hakumaliza mchezo huo, aliumia na kutolewa.
Baada ya hapo akapewa mkataba, kilichofuata ni kuwa hakuonyesha uwezo wa juu kama ilivyotegemewa licha ya kupewa nafasi na kocha wake, Hans van Der Pluijm.
Baadaye akakutana na tukio la kuibiwa mali zake zilizokuwa chumbani katika nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Sinza-Shekilango jijini Dar inadaiwa aliibiwa na ‘kiburudisho’.
 Hapo katikati akazama kwenye penzi la muigizaji wa Bongo Muvi, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, baada ya kudumu kwa muda mfupi, ‘wakamwagana’.
Siku chache baada ya kutengana, Kabula akaibuka katika mitandao ya kijamii na kushusha lugha kali kwa Sherman huku akiweka picha ya mchezaji huyo akiwa kitandani.
Kama filamu vile, siku chache baada ya Kabula kuwasha moto huo, kukaibuka picha zinazomuonyesha Kabula akiwa mtupu akioga. Gazeti hili lilizungumza na wahusika wote kwa nyakati tofauti.
Championi: Kabula unamjua Sherman?
Kabula: Ndiyo namjua, alikuwa mtu wangu lakini siyo kwa sasa, kila mtu yuko kivyake.
Kwa nini ulimtusi kwenye mtandao?
Kabula: Alinitibua na mimi nikaamua kumtusi kupitia Insta.
Unahisi yeye ndiye amehusika na picha zako za utupu?
Kabula: Nashindwa hata nikueleze vipi, sababu kichwa changu nakisikia hakiko vizuri. Sina namna ya kuzielezea picha hizo, kama ni kudhalilika nimeshadhalilika sana, maana kama ni kusambaa kwenye mitandao zimesambaa na kila mmoja anaongea kivyake.
Hata nikitaka nilifafanue naona nitazidi kusababisha makubwa na kuwachongea wengi. Kwa kuwa limeshatokea basi namuachia Mungu, naamini nalo litapita na maisha yataendelea, lakini suala la hizo picha sitaki kumtuhumu moja kwa moja.
Upande wa Sherman ambaye ni raia wa Liberia mahojiano yalikuwa hivi:
Una uhusiano gani na Kabula?
Sherman: Kabula alikuwa mpenzi wangu lakini hatukudumu sana, kwa kuwa nilipata taarifa zake mbaya nikaamua kujiweka kando. Amekuwa akinitafuta ila simtaki na sitaki kumuona.
Kuna picha zake za utupu zimesambaa, unahusika kwa chochote?
Sherman: (Anacheka) Labda akili hazimtoshi, mimi siwezi kufanya upuuzi kama huo. Aseme kweli kama anatafuta ‘kick’ kwangu ijulikane.
Nitakuwa mjinga gani wa kuweka upuuzi wa namna hiyo kwenye mtandao, ndiyo maana niliamua kuachana naye baada ya kuambiwa tabia zake chafu.
Kabla ya Kabula uliwahi kuwa na uhusiano na staa yeyote?
Sherman: Hapana na sitaki kuwasikia tena.
Lakini kuhusu…
Sherman: (Anamkatisha mwandishi) Hakuna kitu kama hicho (Inadaiwa kuwa aliwahi kuwa ‘karibu’ na Dokii na Snura).

Thursday, May 21, 2015

MSIKIE MSANII PIPI AKIFUNGUKIA NGOMA YAKE MPYA ALIYOFANYA NA BARNABA

JOHARI NILIKUWA MAMA NTILIE!

 
Brighton masalu KABLA hajaanza ‘kuuza sura’ kwenye runinga, Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’ alikuwa akijihusisha na kazi ya upishi na uuzaji wa chakula biashara ambayo aliifanya jijini Dar kabla hajajiunga na Kundi la Sanaa la Kaole baada ya kuhitimu mafunzo ya Hotel Management.
 
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’.
Johari alianza kupika na kuuza chakula kwenye catering ya shangazi yake huku akihangaika kutafuta njia ya kutimiza ndoto yake ya uigizaji aliyokuwa nayo tangu akiwa kijijini kwao Bugoyi mkoani Shinyanga.Johari anasema aliamua kusomea masomo ya upishi kwa kushinikizwa na ndugu zake walioamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kupika chakula kizuri na kitamu japo moyoni mwake hakuwa na ‘hobi’ hiyo.
“Kabla ya kutimiza ndoto yangu hii ya uigizaji, nilikuwa napika na kuuza chakula, si unajua katika maisha kabla hujatimiza ndoto na malengo yako ni lazima uhangaike kwa kupitia vikwazo na vizingiti vingi?
“Hivyo mimi nilijikuta nikiangukia kwenye u-hotelia japo sikuwa interested kabisa, lakini kwa sasa namshukuru Mungu kwa kuwa nimetimiza ndoto yangu,” alisema Johari katika mahojiano maalum na mwandishi wetu hivi karibuni.

MADAI JINI KABULA AREKODIWA

SHABAAASH! Staa aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, anadaiwa kurekodiwa mkanda wa ngono na kusambazwa katika mitandao ya kijamii, Amani linakupa stori kamili.
Staa aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
Chanzo cha habari hii kimeeleza kwamba, tukio hilo lilitokea hivi karibuni baada ya mtu anayedaiwa kuwa ni mchumba wa staa huyo kumrekodi video hiyo na baadaye walipopishana kauli, akaamua kuisambaza kwa njia ya CD.
“Jana bwana niliona video ya utupu ya Jini Kabula ikiuzwa kitaani kwetu katika CD jambo ambalo ni aibu sana,” alisema mtoa ubuyu wetu, mkazi wa Manzese, jijini Dar.
Amani lilishuhudia baadhi ya picha zinazodaiwa kuwa zilikatwa kutoka katika video hiyo ndipo mwanahabari wetu alipomvutia waya Jini Kabula ili kujua nini kilimsibu hadi akarekodiwa video hiyo.Alisema kwa mazingira ya tukio hilo, anashindwa hata ajibu nini maana haelewi kilichotokea hadi mkanda huo ukasambaa kiasi hicho na kumsababishia matatizo kwa ndugu zake.
“Kiukweli nashindwa hata nikujibu nini maana kama aibu tayari imeshanikuta, hivyo sioni kama naweza kuongea kitu chochote kwa sasa kikanisafisha, kikubwa namwachia Mungu maana sina tena pa kuuficha uso wangu kwa hiki kilichotokea, yaani yamenikuta,” alisema Jini Kabula ambapo alipobanwa zaidi kuhusu aliyemrekodi, alijibu kuwa ni mchezaji wa timu ya Yanga pasipo kumtaja jina.
“Bwana ni mchezaji wa Yanga, alikuwa mtu wangu.”

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...