Wednesday, April 25, 2012



Mshauri wa Huduma Umoja wa Mataifa nchini Bw.George Otoo akifanya Presentantion juu ya ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mawasiliano kwa Maafisa Mawasiliano na Uhusiano waliohudhuria mafunzo hayo.


Na. Mwandishi wetu


Umoja wa Mataifa umesema Tanzania ni mshirika wake wa karibu katika jitihada za kukuza na kuendeleza sekta ya mawasiliano ambayo ndio kiungo muhimu katika kutimiza majukumu ya kila siku ya idara na taasisi mbali mbali za serikali na hata binafsi.


Akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou, wakati wa warsha ya siku moja ya mafunzo kwa maafisa uhusiano wa wizara na taasisi za kiserikali ilifanyika leo jijini Dar es Salaam, Kaimu wa Mwakilishi Mkazi Dkt. Julitta Onabanjo amesema UN inaitambua Tanzania kama nchi mfano wa kuigwa na itakayonufaika kwa kufuata mikakati ya kutimiza malengo.


Aidha amepongeza namna ushirikiano baina ya UN na Tanzania unavyokwenda haswa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya mashirika tofauti ya Umoja huo na jinsi fedha za misaada zinavyotumika.


Naye Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nchini Tanzania Bw. Salva Rweyemamu amesema mafunzo hayo yamefanyika wakati muafaka ambapo taifa linakabiliwa na changamoto mbali mbali katika sekta nyeti ya mawasiliano.


Amefafanua kuwa mawasiliano ni nyanja muhimu katika utawala na uongozi wa nchi na pia katika kuimarisha uhusiano wa kimatifa na nchi nyinginezo.


Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na United Nations communication Group kwa kupitia Ofisi ya Rais na kuwashirikisha maafisa uhusiano na maafisa mawasiliano kutoka Wizara, Idara na Taasisi kadhaa za serikali.


Bw. Owaiss Parray kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) akifafanua Mipango ya kazi na njia za utekelezaji wake na jinsi zinavyohusiana na masuala ya mawasiliano.

Bw. Yusuph Al Amin kutoka Umoja wa Mataifa nchini akichambua vipengele vinavyohusiana na jinsi mawasiliano zinavyoweza kuchangia maendeleo.

Mtaalam wa masuala ya Teknolojia ya Habari Bw. Ayub Rioba akitoa somo kuhusiana na mipango na mikakati ya Serikali ya Mawasiliano ambapo pia alizungumzia juu ya umuhimu wa kufata maadili wakati wa kufanya mawasiliano katika semina ya mafunzo ya siku moja kwa Maafisa Mawasiliano wa Idara mbalimbali za Serikali.



Kaimu wa Mwakilishi Mkazi Dkt. Julitta Onabanjo akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Uhusiano wa Wizara mbalimbali nchini iliyoandaliwa na United Nations Communications Group kupitia Ofisi ya Rais iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nchini Tanzania Bw. Salva Rweyemamu akitoa nasaha na shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo amesema ni muhimu kwa ajili ya kuongeza ufahamu kwa maafisa mawasiliano na Uhusiano wa Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.

COCA-COLA YAZINDUA KAMPENI YA SABABU BILIONI ZA KUITHAMINI AFRIKA

Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi (kushoto) akimkabidhi zawadi ya dekoda, mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Fariji Msonsa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Coca-Cola ya 'sababu bilioni za kuthamini Afrika' Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Dimeji Olaniyan.
Filbert Bayi (kushoto) akimkabidhi zawadi ya dekoda, mwandishi wa habari Agnes Sikaonga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Coca-Cola ya 'sababu bilioni za kuthamini Afrika' Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Dimeji Olaniyan.

... akiiingiza mkono kwenye kasha kuchagua karatasi lenye jina la mshindi wa bahati nasibu iliyochezwa wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mshereheshaji wa hafla hiyo, Kibonde

...akimkabidhi zawadi ya Televisheni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Nora Damiani aliyeshinda bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Coca-Cola ya 'sababu bilioni za kuthamini Afrika' Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Dimeji Olaniyan.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika leo Mlimani City, Dar es Salaam

Wanahabari wakiwa kazini wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
PICHA/HABARI: JANE JOHN/BLOG



Kocha wa mchezo wa Masumbwi Abdalah Ilamba 'Komandoo' akimfanyisha mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo bondia Francis Cheka Dar es salaam jana Chaka anajiandaa na mpambano wake na Mada Maugo utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo mshindi atakuwa bingwa wa Mkanda wa I.B.F na atanyakua Zawadi ya gari.

Tuesday, April 24, 2012

KILI TALENTS SEARCH 2012 YARINDIMA DODOMA

Hawa ndio 20 bora waliokuwa wameingia katika fainali za mashindano hayo kutoka mkoani Dodoma

Washiriki wakipongezana baada ya tatu bora itakayowakilisha mkoa wa Dodoma kutajwa

Tatu bora, kutoka kushoto ni halima ramadhani, katikati ni Juma Madaraka na mwisho kabisa ni Issa Dubat

Washiriki wakifurahi pamoja baada ya washindi kutajwa
PICHA: JANE JOHN BLOG
BINGWA wa kick Boxing. Japhet Kaseba amesaini mkataba wa kucheza na
Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Kaseba amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mapambano

;Najua mabondia wa hapa bongo wananikwepa sana kwa kuwa nimeshakuwa bingwa wa ngumi za mateke lakini awajui mimi ni bingwa katika mapigano yote alisema Kaseba;


Nitahakikisha naweka kambi ya kutosha na kukata ngebe za cheka ni mtoto mdogo sana katika masumbwi kwa kweli bingwa wa kweli ni Rashidi Matumla ambaye ninamuheshimu mpaka sasa cheka kanikimbia mda mrefu tu tangia tupambane 3 October 2009 ambapo alipewa ubingwa kwa kusingizia mshabiki wangu alikuja kumtupa nje ya uwanja kazi yake yeye anarudiana na Mada Maugo kila siku lakini kwa sasa kakanyaga miwaya zamu yake imefika,

Nae Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi


Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae;
WASANII WA BONGO FLEVA WAPEWA DARASA



    Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha muziki wa asili nchini, Che Mundugwao akiongea na wadau wa Jukwaa la Sanaa (hawako pichani) wakati akiwasilisha mada iliyohusu Utunzi na Ubora Katika Tungo za Muziki. Kulia ni Maafisa kutoka BASATA, Aristide Kwizela na Agnes Kimwaga.
  

Na Mwandishi Wetu
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wameshauriwa kuwa na msimamo katika aina ya mahadhi ya muziki wanaoimba kuliko ilivyo sasa ambapo wengi wamekuwa wakichanganya na kushindwa kueleweka.
Wito huo umetolewa wiki hii na wadau wa Sanaa wakati wakiongea kwa nyakati tofauti kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo walisema kuwa, halil hiyo imeufanya muziki wetu ukose utambulisho na kushindwa kufanya vizuri kimataifa.
“Wasanii wetu wamekuwa wakichanganganya mahadhi (aina) ya muziki wanaoimba.Leo anaimba reggae, kesho zouk mara muziki wa asili, hii inamfanya msanii asieleweke aina ya muziki anaoimba lakini pia tunakosa ubobezi kwenye aina hizi” alisema Che Mundugwao ambaye ni makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki nchini.
Aliongeza kuwa, kubadilika-badilika kwa wasanii kwenye aina ya muziki wanaoufanya si tu kumeufanya muziki wetu ushindwe kuvuma kimataifa bali pia unakosa utambulisho kwenye aina zingine za miziki zinazopatikana na kufahamika duniani kote.
“Muziki ni lugha ya Dunia, aina zake zinafahamika duniani kote.Tunachopaswa kufanya ni kutumia vionjo vya asili yetu ili kuleta utofauti. Tusipofanya hivyo tutaendelea kuwatumbuiza watanzaia wenzetu waishio ughaibuni tu na si kufanya matamasha ya kimataifa” alisistiza Che Mundugwao ambaye pia ni msanii wa muziki wa asili.
Mdau mwingine aliyefahamika kwa jina la Mbile Hango alionya kuwa, wasanii wetu wataendelea kuvuma kwa muda mfupi na kutoweka kama hawatazingatia taaluma na ubobezi katika aina fulani ya muziki.
Aliongeza kuwa, ni vigumu kwa wasanii kuimba kwa kunakiri muziki kutoka nchi za nje kama ile ya qwaito yenye asili ya Afrika Kusini halafu wategemee kupata fursa ya kuuza kazi zao nje na kushiriki matamasha ya kimataifa.
“Ukinakiri muziki kutoka nje maana yake huna kipya cha kupeleka nje, tutaendelea kuvuma humu humu ndani” alionya.
Mjadala wa wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa ulijikita kwenye Ubora katika Utunzi wa Tungo za Muziki




Mkongwe wa Muziki wa dansi nchini, Mzee Kassim Mapili akichukua notisi ya kile kinachojadiliwa kwenye Jukwaa la Sanaa. Aliwaasa Wasanii kujifunza na utunzi wa ala katika muziki.



Mdau akichangia mjadala kwa hisia.

Monday, April 23, 2012

RAY: NIMECHOKA KUKAA KIMYA, NAOMBA NIELEWEKE KUWA SIHUSIKI NA KIFO CHA KANUMBA




YAPATA wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia, na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbali mbali kutokana na mitazamo ya watu kupishana kuhusiana na jambo husika. Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo, hususan mazingira ya kifo chake; kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba), na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho, kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine ninahusika na mauaji ya Steven Kanumba. Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu, nimekuwa nikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho, kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi ya mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira, ila kuna ukweli usemao kwamba, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli, nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.
Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwanza kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadae ulisababisha kifo chake. Na na hata nilipofika katika hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake; ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndio maana hata Polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakuna mazingira yoyote yanayonihusisha mimi na kifo hicho.
Pili, watu wanahusisha tofauti za kibinadamu zilizokuwepo baina yetu na kifo hicho, nasema hii sio sahihi kwa sababu kwanza ni kawaida kwa binadamu kutofautiana, isipokuwa kwetu sisi baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vinakuza kwa sababu nisizozijua, hivyo jamii ikachukulia kuwa tofauti zile ni uadui kitu ambacho sio sahihi, kwani sisi hatukuwa watu pekee tunaotofautiana kwani huu ni mwenendo wa kawaida wa dunia; hivi jana tumeshuhudia Waziri mmoja akieleza bayana katika mkutano na waandishi wa habari kuwa na tofauti na naibu wake, lakini hatuajasikia ikiandikwa wana ‘bifu’ bali imetafutwa lugha nzuri ya kupamba tofauti hizo, kwa kuwa waliohusika ni waheshimiwa, ila kwa wengine kutokana na sababu tusizozijua, inaonekana kama ni haki yetu kuandikwa vibaya. Kinachosikitisha, kwa nini jambo hili linachukuliwa kwa mkazo mkubwa sana, kwani hatujawahi kusikia watu wakiwa wanatofautiana na ndugu jamaa hata na marafiki zao na inaonekana kawaida tu? Kwani vyombo vya habari havikuwahi kuandika kuwa marehemu Steven Kanumba alikuwa na tofauti na baba yake, na yeye mwenyewe alitamka hivyo katika vyombo vya habari, mbona wameliongea bila kuongeza chumvi, na jamii inaona kuwa ni jambo la kawaida la kibinadamu.
Pengine watu wanaojaribu kuongea hayo, hawajui mimi na Steven Kanumba tumetoka wapi? Sisi si watu tuliokutana barabarani, tuna historia katika kazi yetu ya sanaa na pia katika maisha maisha yetu. Mwanzoni kabisa, mimi ndiye niliyempokea Kanumba pale Kaole na ndiye niliyemfundisha sanaa pale (nadhani watu wanakumbuka tamthiliya za wakati huo ITV) na baada ya hapo tulienda pamoja katika kampuni ya Game 1st Quality pamoja na tukafanya filamu kama Johari, Sikitiko Langu, Dangerous Disire na nyinginezo, na tuliendelea kuwa pamoja katika kampuni hiyo mpaka tulipofanya filamu ya Oprah mwaka 2008 ambapo niliingia rasmi kufanya kazi za kampuni yangu, lakini tuliendelea kuwa pamoja hata wakati nikiendelea na kazi za kampuni yangu. Pia mimi nilikuwa wa kwanza kuanza kufanya kazi na Steps na baadae Kanumba alipoanza kufanya kazi zake mwenyewe na kunikuta huko tuliendelea kuwa pamoja kama siku zote. Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu, ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu, Isitoshe hata vitu vyetu binafsi utaona kama kuna kufanana; kuna wakati Kanumba alinunua Toyota Ruv 4 nyeusi mimi nikanunua ya kijani, aliponunua Harrier na mimi nikanunua pia, na hata gari za hivi karibuni, ukitazama utaona kuwa zinafana kwa karibu; hii ilikuwa ni kama maisha yetu, hatukuwa na uadui, ilikuwa tunapeana changamoto za maendeleo.
Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndio maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui, kuna watu ambao wanafanya kazi nami katika kampuni yangu ya RJ ndio hao hao Kanumba alikuwa anawatumia siku zote katika kazi zake, hata baada ya tofauti hizo hakuna aliyekoma kufanya kazi na yeyote kati yetu. Hii inathibitisha kuwa tofauti ilikuwa kati yetu kama binadamu, sio chuki za kimafanikio, ingekuwa hivyo watu kama Junior Syaary ambaye mara nyingi hufanya final editing katika RJ ndio huyo huyo alikuwa akifanya na Kanumba, Ally Yakuti ambaye anaandika script za RJ, ndiye huyo huyo aliyekuwa anaandika kwa Kanumba, Steven Shoo ambaye ni mtaalamu wangu wa light, ndiye huyo huyo anayetumiwa na Kanumba na wengine wengi kama Juma Chikoka aliyecheza kikamilifu katika filamu ya kijiji cha Tambua Haki, ambaye pia anashiriki filamu nyingi za RJ, na wote hao, hawakuanzia kwa Kanumba, wote wameanza kwangu mimi ndio niliompatia na hata baada ya hayo yanayosemwa kuwa kuwa ni uadui, sikuwahi kuwakataza kufanya kazi na Kanumba.
Tatu kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje. Napenda kusema wazi wazi kuwa, kwa kila anayetekwa na wimbi hili, ajaribu kufikiria leo ipo kwangu mimi, kesho inaweza kuhamia kwako, kwani mimi sio wa kwanza kufikwa na haya, inaweza kukukuta hata wewe au ndugu yako, utajisikiaje. Na kama kweli mimi nimehusika na kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile, basi Mungu atanihukumu na kila aliye hai atashuhudia, ila kama sijahusika kwa lolote, Mungu hatonihukumu na badala yake ataniinua, kwa kuwa ninapita katika kipindi kigumu mno sasa hivi kwa madhila haya.
Mwisho kabisa napenda kumaliza kwa msemo usemao, ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke, kwani kadri mambo haya yanavyoendelea, usidhani yataishia kwangu, kwani mkono wa dhuluma haushii karibu, ukisikia jirani anapiga kelele za mwizi, usilale kamsaidie, usiseme kuwa hatuhusiki kwani hayupo kwetu, kesho utafikwa na wewe utakosa wa kukusaidia. cha msingi kama tunampenda sana ndugu yetu ni kumuombea kwa Mungu, kwani hatujui makao yake huko aliko, na sio kuunda vitu ambavyo kamwe hata yeye angekuwa hai asingeviafiki.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA MAHALI PEMA
PEPONI
MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA
KESI YA LULU YAZIDI KUSOGEZWA MBELE 

 

Mshitakiwa wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii wa filamu Bongo Steven Charles Kanumba, 'Kanumba The Great',  Elizabeth Michael 'Lulu', akisindikizwa na Askali Magereza tayari kwa  kupandishwa Kizimbani kwa maranyingini ili kutajwa na kusomewa  mashitaka juu ya kesi inayomkabili ingawa  kwa mujibu wa wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda, kesi hiyo imesogezwa mbele  kwa madai ya  upelelezi kutokamilika hivyo kuahirishwa tena mpaka  Mei 7 mwaka huu itakapotajwa upya.

Baadhi ya wapiga picha na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliofika Mahakamani hapo wakijaribu kuchukua data za tukio zima la kesi hiyo.

Sunday, April 22, 2012



Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Epraim Mafuru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Promotion ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO kupitia bia tatu za Serengeti, Tusker na Pilsner Lager na washindi kujizolea zawadi mbali ambapo zawadi za Shilingi Milioni 700 kushindaniwa. Pamoja nae Kulia ni Mkuzaji wa M PESA kutoka Kitengo cha Biashara, Asia Natalia Mhina na Kushoto ni Meneja wa Bia ya Pilsner Lager, Maurice Njowoka.
KAMPUNI ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia vinywaji vyake bora kabisa vya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager iameandaa promosheni kubwa na ya aina yake itakayofanyika Tanzania nzima katika kipindi cha wiki 16 ambapo zawadi mbalimbali zitashindaniwa.


Promosheni hiyo ya aina yake imesheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile Jenereta 16 , Pikipiki 8, Bajaji 8, Gari ndogo maarufu kama saloon car 8, pamoja na zawadi zingine nyingi ambapo kila baada ya wiki mbili gari 1 aina ya saloon itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki mbili Bajaji 1 itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki Pikipiki moja itashindaniwa na kila baada ya wiki moja Jenereta moja itakuwa inashindaniwa.



Akizungumzia promosheni hiyo kabambe Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, bwana Ephraim Mafuru amesema promosheni hiyo sio tu inalenga kuongeza mauzo ya vinywaji hivyo bali pia inalenga kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania hususani wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ikiwa ni sera mojawapo ya kampuni hiyo kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia bidhaa zake zenye ubora wa aina yake.



“Kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya taifa letu katika maeneo mbalimbli kupitia jamii inayotuzunguka na wateja wetu kimaisha, hivyo promosheni hii pamoja na ukweli kuwa inalenga kuongeza tija katika masoko ya bidhaa zetu bado unaweza kuona zawadi zitakazoshindaniwa katika promosheni hii ni zawadi kubwa ambazo kwa namna moja ama nyingine inaweza kubadilisha maisha ya mshindi wetu kutoka hatua aliokuwepo hadi hatua nyingine, kwa hivyo sisi SBL tunasema tunajivunia kuwa sehemu mojawapo inayochangia maendeleo ya watanzania wateja wetu na taifa kwa ujumla” alisema bwana Mafuru.



Kwa upande wake Meneja wa bia ya Tusker Lager, Bi Rita Mchaki, amesema kampuni ya bia ya Serengeti inazalisha bidhaa zinazopendwa na watanzania wengi kutokana na ubora wa kipekee wa bidhaa hiyo, na kwamba promosheni hiyo kabambe nisawa nakurudisha shukrani zake kwa watanzania kwa kufanikisha kampuni hiyo kufikia malengo yake kibiashara.

Watanzania wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi na wanaotumia bidhaa zetu zilizoainishwa katika promosheni hii wanaombwa kushiriki kwa wingi bila kukata tamaa kwani zawadi zinazoshindaniwa zinaweza kubadilisha maisha kwa yeyote atakayebahatika kuibuka na ushindi.


MAELEKEZO: Nunua bia ya serengeti lager, Tusker lager au Pilsner Lager fungua kisha bandua ganda lililo ndania ya kizibo utapata namba zilizopo katikati ya kizibo, Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako, nakili namba hizo mfano 55550, kisha tuma namba zilizopo pembezoni mwa kizibo. Fanya hivyo kwa kufuata maelekezo katika vipeperushi na magazeti.unaweza pia kijipatia bia ya bure papo hapo kila ubanduapo kizibo cha bia ziliainishwa katika promosheni hii.



Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Epraim Mafuru (katikati) akionesha zawadi mbali mbali zitakazo tolewa katika Promotion hiyo ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO kupitia bia tatu za Serengeti, Tusker na Pilsner Lager na washindi kujizolea zawadi mbali ambapo zawadi za Shilingi Milioni 700 kushindaniwa. Zawadi zitakazo tolewa ni pamoja na Fedha Taslimu, Bia za Bure, Jenereta, Bajaji, Pikipiki na Gari aina ya Figo. Mafuru amesema Promosheni hii itadumu kwa Wiki 16 kuanzia Jumanne Aprili 24,2012. Kulia ni Mkuzaji wa M PESA kutoka Kitengo cha Biashara, Asia Natalia Mhina.



MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. Zuwena Kibena ' Mama Kanari Kipingu' akikabidhi pesa ya maji kwa Nahodha wa timu ya Taifa ya masumbwi Selemani Kidunda wachezaji wa timu hiyo jana



MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. zUWENA Kibena ' Mama Kanari Kipingu' kushoto akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Masumbwi alipotembelea kambi yao iliypo Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani juzi na kutoa ahadi mbalimbali kwa mabondia hawo.

MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. zUWENA Kibena ' Mama Kanari Kipingu' kushoto akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Masumbwi alipotembelea kambi yao iliypo Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani juzi na kutoa ahadi mbalimbali kwa mabondia hawo.
WANACHAMA WA GEPF KULIPA MICHANGO YAO KWA NJIA YA AIRTEL MONEY


Meneja wa kitengo cha Airtel money Asupya Nalingingwa akielezea huduma za
Airtel money na urahisi wa wanachama wa GEPF kuchangia kwa kutumia Airtel
money katika halfa ya uzinduzi iliyofanyika katika hotel ya Gold crest ,
Pichani kulia ni Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal  akisikiliza
maelekezo hayo.


Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal akikata utepe ikiwa ni ishara ya
kuzindua mfumo wa malipo ya michango ya wanachama wa GEPF kwa kupitia
huduma ya Airtel money,halfa fupi ya  uzinduzi huo ulifanyika  katika hotel
ya Gold Crest Mwanza. Kushoto ni Meneja wa kitengo cha Airtel money Asupya
Nalingingwa, akifatiwa na Naibu Waziri wa fedha mh. Gregory Teu,na kaimu
mwenyekiti wa bodi bw Ladislaus Salema.






 Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal akikata utepe ikiwa ni ishara ya
kuzindua mfumo wa malipo ya michango ya wanachama wa GEPF kwa kupitia
huduma ya Airtel money, uzinduzi huo ulifanyika katika halfa fupi
iliyofanyika katika hotel ya Gold Crest Mwanza. Kushoto ni Meneja wa
kitengo cha Airtel money Asupya Nalingingwa, akifatiwa na Naibu Waziri wa
fedha Mh.Gregory Teu,na kaimu mwenyekiti wa bodi bw Ladislaus Salema, kulia
ni menaja masoko GEPF Aloyce Ntukamazina, akifatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa
GEPF Daud Msangi akifatiwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng Evarist Ndikiro.



Meneja wa kitengo cha Airtel money Asupya Nalingingwa akimshukuru Makamu wa
Rais Dr Mohamed Gharib Bilal mara baada ya kuzindua mfumo wa malipo ya
michango ya wanachama wa GEPF kwa kupitia huduma ya Airtel money, uzinduzi
huo ulifanyika katika halfa fupi iliyofanyika katika hotel ya Golden Crest
Mwanza. Pichani ni viongozi na wajumbe wa GEPF pamoja washiriki wa halfa
hiyo.


 
Meneja wa kitengo cha Airtel money Asupya Nalingingwa akiongea na waandishi
wa habari akifafanua juu ya mpango maalumu uliozinduliwa utakaowawezesha
wanachama wa GEPF kulipa michango yao ya mwenzi kwa kupitia huduma ya
Airtel money. Halfa ya uzinduzi imefanyika katika hotel ya Gold Crest
Mwanza.

Thursday, April 12, 2012

LULU KAFUTA NDOTO ZA STEVEN KANUMBA KUWA MBUNGE


Hayati Steven charles Kusekwa Kanumba gwiji la filamu alieuwawa hivi karibuni nyumbani kwake sinza maeneo ya vatican,ndoto za msanii huyu kuwa mwanasiasa mashuhuri zilitoweka baada ya mtuhumiwa Lulu kudaiwa kumua wakiwa chumbani kwake.

Steven Kanumba alikuwa na mkakati wa kugombea ubunge mkoani shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Democrasia na maendeleo (CHADEMA) na alikuwa mfuasi wa chama hiko kwa siri kubwa na hakutaka watu wajue hususani viongozi na wanachama wa (CCM) kwani alikuwa nao karibu sana na hakutaka kuaribu ukaribu nao mapema kabla hakijafika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015.
Kanumba alikuwa ni rafiki(best friend) na msiri wa Magese kwani alikuwa kanizoea kiasi cha kuniambia mambo mengi hususani maisha na maswala ya mahusiano kati yake na watu aliokuwa nao katika nyakati tofautitofauti The great alikuwa hanifichi kitu panapo ukweli aliniambia bila woga tena aliniambia nisimwambie mtu kuhusu jambo hili wala nisiandike kwenye blog kabla wakati haujafika,ila leo nimeamua kusema kwakua rafiki yangu hayupo tena duniani.

Kwa mujibu wa Marehemu Kanumba alipewa msukumo zaidi wa kuanza kujiandaa kua mgombea ubunge kwa tiketi ya (CHADEMA) na Mh.Zitto kabwe ambae ni rafiki mkubwa wa marehemu Steven kanumba,nasehemu ambayo kanumba alikuwa kanuia kujitosa kichwa-kichwa ni nyumbani kwao Shinyanga sehemu ambayo ndiko chimbuko lake.

Pamoja na kuhamasika kwa mchakato wa kuwania ubunge 2015 kanumba aliniambia hivi "kaka hata kama nikiwa mbunge siachi kutoa movie ntakua najitaidi japo nitoe hata moja tu kwa mwezi,kipindi ambacho ntakuwa siko bungeni ntapiga shooting(clip) zakufa mtu..nyingi ili nikiingia mjengeni naedit tu" alimaliza steven.

Kanumba hakutaka watu wengi wajue adhima yake hii ya kuwa mbunge 2015 kwani alijua akisema mapema watu wangemvunja moyo,wengine wangeanza kumwalibia mapema na hakutaka kuitarafiana na viongozo wa CCM mapema ambapo wengi wao ni viongozi wa juu na wengi wao hukaa nao vikao nyeti na humwamini sana kuwa ni mwanachama wa CCM.

Marehemu aliniambia maneno haya nyumbani kwake Sinza Vatcan moja ya siku ambapo aliniita nyumbani kwake tukaongea sana kama ilivyokuwa desturi yetu siku akiniona hunipa michapo mingi hasa yale mambo yetu ya ujana zaidi.

Magese ntamkumbuka sana Kanumba kwani ni kati ya watu walionisapoti sana katika harakati zangu watanzania wengi wanakumbuka hii,kashatoa fedha nyingi,muda mwingi katika harakati zangu na hakuitaji nimlipe hata shilingi moja toka kwangu,alinithamini kama ndugu yangu wa damu.
Moja ya kauli ambayo sitaisahau aliniambia "Ndugu yangu magese fanya kazi kwa bidii jitume usikate tamaa....hata kama ungekuwa mfagiaji....fagia kwa moyo na uipende kazi yako kwani katika kufagia vizuri ipo siku unaweza kuchaguliwa mfagia ikulu...katika kufagia huko utakuwa umeinuliwa toka ngazi moja kwenda nyingine" alisisitia The great.

R.I.P STEVEN KANUMBA , amen.

Wednesday, April 11, 2012

MAREHEMU STEVEN KANUMBA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI KWA HESHIMA KUBWA, KWELI ALIKUWA MTU WA WATU

Waombolezaji wa msiba wa Marehemu Steven Charles Kanumba wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu kwenye kaburi, tayari kwa kumpumuzisha katika nyumba ya milele kwenye makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo jioni , Kanumba atakumbukwa kwa kazi yake nzuri katika tasnia ya filamu hapa nchini, ambapo alijitangaza na kuitangaza nchi vyema ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kupitia filamu zake nyingi alizoigiza.
(MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN)
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa na ndugu wa karibu wakiaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho makaburini Kinondoni.
Waombolezaji wakitayarisha jeneza la marehemu Steven Kanumba tayari kwa kuliweka kaburini.
Mmoja wa waombolezaji akibebwa baada ya kupoteza fahamu makaburini.
Wajenzi wa kaburi la marehemu wakichanganya Sementi kwa ajili ya kufukia.

Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa akiuaga mwili wa mwanaye kwa mara ya mwisho kabla ya kuzikwa rasmi katika makaburi ya Kinondoni.
Wafanyakazi wa msalaba mwekundu wamefanya kazi ya ziada kutoa huduma ya kwanza kwa waombolezaji
Polisi wakiweka ulizi wa kutosha katika mazishi hayo.

Mwanamitindo maarufu mtanzania anayefanya kazi zake za mitindo nchini Marekani Millen Magese akienda kuweka shada la Maua kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba.
Mama wa Marehemu Steven Kanumba akiweka shada la maua mkaburini
........BABA WA KANUMBA ASHINDWA KUHUDHURIA MAZISHI YA MWANAE.......SHIBUDA AMWAKILISHA.......
MBUNGE wa Maswa Magharibi, John Shibuda jana alimwakilisha baba wa msanii maarufu wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba katika mazishi ya msanii huyo akidai kuwa baba huyo Charles Kusekwa Kanumba ameshindwa kuhudhuria mazishi hayo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya malaria na shinikizo la damu na si matatizo yake na merehemu huyo. Kupitia uwakilishi huo, Shibuda pia alisoma barua aliyoeleza kutoka kwa mzazi huyo wa Steven Kanumba akieleza kushindwa kwake kufika kwenye mazishi hayo na kwamba ametuma watoto wake na wakwe zake kumwakilisha. "Baba yake Kanumba siku ya Jumamosi alikuwa anajisikia vibaya na alipokwenda hospitali alipimwa na kukutwa ana malaria 15 na shinikizo la damu likiwa 180 - 140. Lakini pia ana matatizo ya miguu kwa muda mrefu, anatembea kwa msaada wa baiskel,"alisema Shibuda. Akisoma barua hiyo Shibuda alinukuu barua ya baba wa Kanumba akisema:"Salam, nashukuru wana kamati ya mazishi ya mwanangu kwa kunitumia nauli ili niweze kuja kumzika mtoto wangu. Lakini kutokana na maradhi yanayonikabili sitaweza kuja, ila nawatuma wanangu Michael na Mjanael, pia mkwe wangu Chrisant Msipi waniwakilishe. Matatizo yangu na mwanangu yalishakwisha." "Msianze kuleta maneno yenu ya umbea umbea na uzushi eti hajafika kwenye msiba wa mwanawe kwa kuwa hawaelewani huo ni uzushi, walishaelewana na alikuwa na mawasiliano mazuri na mke wake mama Kanumba na ndiyo maana akatuma wawakilishi wake,"alisema Shibuda.

Friday, April 6, 2012

HUYU NDIYE ALIYEIGIZAJI FILAMU YA YESU

Brian Deacon akiigiza kama Yesu ndani ya filamu ya JESUS.

Ikiwa leo ni Ijumaa kuu,siku ambayo wakristo ulimwenguni wanakumbuka mateso ya mkombozi wa ulimwengu Yesu Kristo aliyekuja duniani takribani miaka 2000 iliyopita.Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu.  Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.



Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.



watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.
Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.


Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi
Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku

Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.



Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel.
habari kwa msaada wa mtandao.

Tuesday, April 3, 2012

WANAMITINDO WA BONGO WASHIRIKI ONESHO LA MAVAZI LA WIKI AFRIKA KUSINI


Baadhi ya wabunifu hao wakipita jukwaani  kuonyesha moja ya vazi lao.

 Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Rita (wa tatu kushoto), akiwa katika pozi na baadhi ya wabunifu wa mavazi hayo.
WABUNIFU wa mavazi watatu watanzania wanaoshiriki onesho la wiki ya mavazi Afrika Kusini wametia fola katika onesho hilo.

Wabunifu hao walishiriki onesho hilo kufuatia mwaliko wa mwanamitindo mahiri Millen Magese ambapo walionesha katika shoo iliyoitwa Tanzania International Fashion Exposition (TIFEX).

Wahudhuriaji waliofika kuona shoo ya watanzania hao walikuwa wengi na walivutiwa zaidi na namna ambavyo walichanganya kitenge katika kupendezesha mavazi yao.

Mbunifu Evelyn Rugemalila ndie alifungua pazia kwa kuonesha mavazi yake aliyoyanakshi kwa kanga, aliweza kuzikonga nyoyo za washabiki na kujikuta wakimpigia makofi mara alipomaliza shoo yake.

Kitu ambacho alikifanya tofauti na wabunifu wengine ni wakati anamalizia shoo yake alitembea jukwaani akiwa amewavalisha sare ya nguo za kanga iliyofanana na yake huku.

Baada ya Evelyin kuonesha ilifika zamu ya mbunifu wa mavazi Jamila Swai kuonesha mavazi yake ambapo aliongozana na mbunifu wa mikoba kutoka mradi wa Fahari wa Zanzibar Julie Lawrence.

Wanamitindo wa kizungu na kiafrika wakiongozwa na mwanamitindo mahiri nchini Millen Magese waliwakilisha vema ambapo kila alipokuwa akitokea Millen watu walishangilia.

Baada ya Jamila alifuata Doreen Noni aliwakilisha lebo yake ya Eskado Bird alifuata ambapo naye alitumia viashiria vya kanga pamoja na ngozi ngozi katika nguo zake.

Kwa pamoja wabunifu wa Tanzania walifanya vema katika onesho hilo huku wanamitindo nao wakiwa wamejitaidi kuonesha umahiri katika kutembea.



Mwanamitindo huyo akikatiza jukwaani.



POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...