Tuesday, August 12, 2014

MCHEKESHAJI MAARUFU WA MAREKANI AJIUA

Muigizaji na mchekeshaji maaarufu wa Marekani, Robin Williams amejiua. Mwili wake umekutwa nyumbani kwake California, Marekani Jumatatu Agosti 11, 2014.
Muigizaji na mchekeshaji maaarufu wa Marekani, Robin Williams enzi za uhai wake.
Robin Williams akiwa na mke wake wa tatu, Susan Schneider.
Maua na ujumbe wa kumkumbuka Robin Williams.
Imeelezwa kuwa kwa siku za hivi karibuni Williams ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 63 alikuwa akipambana na sonona.
Muigizaji huyo alikuwa hajitambui na hakuwa anapumua na hivyo kubainika kuwa alijiua kwa kukosa hewa. Williams alionekana nyumbani kwake mara ya mwisho mida ya nne usiku siku ya Jumapili.
Robin alipelekwa rehab mwezi uliopita kujizuia kunywa pombe. Alikuwa akihangaika kuacha kutumia cocaine na pombe katika miaka ya 80 lakini hakuwahi kunywa kwa miaka 20.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...