Friday, September 12, 2014

Mfungwa apatikana na simu mwilini Kenya








Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti ya nyuma.

Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o katika jimbo la Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo ambazo alikuwa amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma. Mfungwa ambaye alitolewa simu mwilini kwa kufanyiwa upasuaji

Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.

Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.

Maafisa wa magereza wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...