Monday, March 30, 2015

DIAMOND, ZARI HATARINI KUMALIZWA

 
TAHADHARI ichukuliwe! Habari zikufikie kuwa, baada ya staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz‘ na mpenzi wake, Zarinah Hassani ‘Zari’, kuhamia kwenye mjengo wake mpya uliopo Madale jijini Dar, imebainika kuwa familia hiyo inaishi roho mkononi kufuatia ulinzi sifuri, jambo linalowafanya kuishi kwa hofu tupu.
Nyumba mpya ya Diamond aliyohamia hivi karibuni.
TUJIUNGE NA CHANZO CHA HABARI
Kikizungumza kwa hofu juu ya familia hiyo, chanzo chetu makini kilipasha kwamba, pamoja na Diamond kutumia mamilioni ya fedha kujenga nyumba hiyo ya gharama kubwa, sasa changamoto imehamia kwenye ulinzi na usalama wao.
Muonekano wa eneo ilipo nyuma ya Diamond iliyopo Madale jijini Dar.
“Jamani watu wanampongeza Diamond kwa kuhamia nyumba mpya lakini wale jamaa aisee wanapaswa kuombewa kila kukicha.
“Pamoja na kushusha mjengo wa maana bado changamoto ni juu ya ulinzi wao.
DIAMOND ANAISHI KIZAMANI?

“Huwezi kuamini Diamond bado anaishi kizamani sana na sijui kwa nini anajiamini kiasi hicho wakati anajua wazi kuwa yeye ni staa wa Afrika na hapaswi kuishi kwa ulinzi hafifu.
MAENEO HATARISHI?
“Nasema hivi kwa sababu hata maeneo anayoishi ni hatari sana kwake hivyo anatakiwa kuwa na ulinzi mkali ili tu siku moja asije akafanyiwa kitu ambacho taifa likaingia kwenye hasara ya kumpoteza nyota mkubwa kama yeye.
“Nina uhakika asilimia mia moja Diamond hadi leo hajaanza hata kufanya process (taratibu) za kuchukua silaha (bastola).
“Mimi naijua vizuri Madale ni sehemu ambayo watu huwa wanavamiwa mara kwa mara na wanaishi kwa hofu kama Diamond anavyoishi.
HIKI NDICHO KINACHOMPONZA
“Kitu kingine kinachomponza Diamond ni ishu ya kuweka kila kitu kilichopo ndani kwake mitandaoni. Usione kila mtu anasifia lakini kuna wengine wanavitolea macho.
“Kwa mfano katupia picha za toilet (choo) ambacho kimepakwa dhahabu na kusema kimegharimu shilingi milioni 70.
“Hajakaa sawa akatupia picha za jikoni kwake kuna vitu vingi vya thamani kubwa kila mahali mpaka kwenye korido kuna flat screen (runinga). Huko si ni kuwakejeli watoto wa mbwa? Ni vizuri akaacha kufanya hivyo kwa sababu anawapa watu tamaa,” kilitiririka chanzo hicho.
ANA ULINZI GANI?
Juu ya ulinzi wa nyumbani kwa Diamond, chanzo hicho kilidai kwamba, mbali na baunsa anayewalinda aitwaye Mwarabu hakuna askari wa silaha anayelinda nyumbani hapo hivyo jamaa anatakiwa kufanya haraka kuajiri walinzi wenye silaha.
BOFYA HAPA KUMSOMA DIAMOND
Baada ya habari hizo na uchunguzi wa kutosha, Ijumaa Wikienda lilimsaka Diamond a.k.a Dangote au Chibu ili kujua namna anavyoishi na jinsi anavyoimarisha ulinzi wake na familia kwa jumla.
Diamond, mbali na kukiri kuwa na hofu, alikuwa na haya ya kusema: “Suala la ulinzi wangu nalijua mwenyewe lakini zaidi watu wanatakiwa kujua mimi nipo na mlinzi na ninaendelea kuimarisha ulinzi wa nyumbani kwangu.
“Sidhani pia kama ni suala zuri sana kwa watu kujua siri za ulinzi wangu ila mambo mengi ya kujilinda niko kwenye michakato ya mwisho kukamilisha na soon (haraka) mambo yote yatakaa levo maana huwezi ukafanya kila jambo kwa wakati mmoja,” alisema Diamond huku akikubaliana na ushauri wa gazeti hili juu ya kuongeza ulinzi alionao wa baunsa.
ILIWAHI KUMTOKEA SUGU
Huko nyuma iliwahi kumtokea Mwanamuziki Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) ambapo alikuwa amerejea kutoka nchini Uingereza.
Akiwa amepanga nyumba nzima maeneo ya Tegeta, Dar, Sugu alifanyiwa makala ya runingani na kuonesha vitu vya thamani vya nyumbani kwake.
Siku chache baada ya kipindi hicho kuruka runingani, jamaa huyo alivamiwa na kuporwa kila kitu lakini yeye hakudhurika

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...