Monday, July 6, 2015

UKAWA wajitoa rasmi Bungeni, waondoka Dodoma leo

Umoja wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza rasmi kususia vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni za bunge.




Umoja wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza rasmi kususia vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni za bunge.
Akitangaza msimamo huo mjini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari, kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Mbowe amesema wabunge wote kutoka katika vyama vinavyounda umoja huo hawataingia tena bungeni licha ya baadhi yao kuwa hawajaadhibiwa.
Umoja huo pia umemtaka Rais Kikwete kutotia saini muswada hiyo kwa kuwa imepitishwa kinyume cha taratibu.
Mbowe amesema kuwa endapo Rais Kikwete atalazimisha kuisaini miswada hiyo, umoja huo utaishitaki serikali kwa wananchi.
Wabunge wote kutoka UKAWA wameazimia kuondoka kabisa leo kutoka mjini Dodoma, na wanataraji kukutana jijini Dar es salaam siku ya Jumatano kwa hatua zaidi.

Wakati huo huo bunge limepitisha muswada wa usimamizi wa mapato yatokanayo na mafuta na gesi, na muswada mwingine wa uwazi na uwajibikaji katika uchimbaji wa madini, gesi na mafuta, hiyo ikiwa ni miswada miwli kati ya mitatu ambayo imekuwa ikipingwa na wabunge kutoka UKAWA.
Muswada mwingine ni ule wa sheria ya Petroli ambao ulipitishwa jana bila ya ushiriki wa wabunge hao.
EATV imefanya mahojiano na Mh. Tundu Lissu mara baada ya kutangazwa kwa msimamo huo wa UKAWA, na hapa anaeleza zaidi:-

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...